Rich Mavoko na Nay wa Mitego wameingia kwenye mzozo mzito...... - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday 11 April 2017

Rich Mavoko na Nay wa Mitego wameingia kwenye mzozo mzito......


Wasanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini, Rich Mavoko & Nay wa Mitego  wamejikuta wakijibizana mitandaoni baada ya Rich Mavoko kutupia picha na maneno yaliashiria ujio wa ngoma yake mpya wakati akisikilizia hali ya kisiasa hapa nchini kwa sasa.

Hitmaker huyo wa Kokoro ameonjesha picha ya kile kinachoonekana kuwa ni video yake mpya na kuandika: ''Haya Mkimaliza Mambo Zenu Za Siasa Mtupe Tarehe Na Sisi Tufumue Hiii #Showme''



Baada ya Post hiyo Saa 18 baadaye, Nay wa Mitego naye akachukua picha ile ile aliyotupia Rich Mavoko, aka-repost na kuandika huku akitamba kuwa ngoma pekee inayoweza kutusua kwa sasa ni ngoma yake ya Wapo. ''NAOMBA MUENDELEE KUSUBILI, MAY BE MPAKA MWAKANI 2018, NDO MTAANZA KUJISHUGHULISHA NA MASWALA YA KUWAIMBIA WANA NCHI''.



Baada ya kutoa maneno hayo, Mwanamuziki Nay wa Mitego alitumia fursa hiyo kwa kumuonya Diamond Platnumz kwa kumtumia salamu zilizosomeka hivi.. ''MWAMBIENI NA BABA YENU PIA AWE MPOLE KWA SASA ALEE WATOTO. KAZI TULIYO NAYO IKIENDA SAWA TUTA WARUHUSU MUENDELEE KUBURUDISHA WANA NCHI. TUNATAKA MAMBO YAENDA SAWA KWANZA''. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here