Aslay Afungukia juu ya Muziki wake na Familia Iliyopo Nyuma Yake - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, 26 October 2017

Aslay Afungukia juu ya Muziki wake na Familia Iliyopo Nyuma Yake


Msanii Anaefanya vizuri katika muziki wa Bongo Flava, Aslay amesema uwepo wa familia nyuma yake ndio kunampa hasira ya kufanya muziki mzuri.

Mkali uyo anaetamba na ngoma wake wa ''Natamba'' Ameiambia XXL ya Clouds Fm wasanii wote ambao wanafanya muziki kutokana na sababu fulani nyuma yao kama hiyo kuna uwezekano mkubwa wa kufika mbali.
''Kwanza kabisa sipendi msanii ambaye anavimba, napenda msanii anayefanya kazi kwa kuonyesha mimi nyuma nina watu wananiangalia,Familia kwa watu kama hao huwa nawaheshimu sana kwa sababu huwa na hasira na maisha halafu ukiangalia kazi zao lazima ziwe nzuri mmoja wapo ni mimi'' amesema Aslay.
Katika hatua nyingine ameongeza kuwa anajitahidi kufanya muziki kwa sababu kuna familia inamtazama na licha kujitahidi ana kipaji pia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here