Msanii wa Muziki wa Hip Hop kutoka kwenye kundi la Weusi, G-Nako amefungukia mafanikio ya cover ya ngoma Seduce Me ya Mwanamuziki Alikiba aliyofanya.
G-Nako a.k.a G-Wala Wala ambaye kwa sasa anatamba na ngoma Energy amepiga story na kipindi cha Clouds E na kufunguka kuwa mapokezi ya ngoma hiyo yamekuwa makubwa sana lakini mambo ya u-team katika muziki Hayafikirii na Hayataki.
''Kwanza kabisa sitaki masuala ya ma-team, kuna vitu kidogo yanakuwa yanatuwekea mipaka, mambo ya team yakae mbali halafu muziki mzuri ndio uongee lakini so far mapokezi ni makubwa nawashukuru fan wangu wote kwa support kubwa walioionesha'' amesema G-Wala Wala.
G-Nako anaungana na producer Man Water na wasanii wengine mbali mbali ambao wamefanya cover ya ngoma hiyo.
No comments:
Post a Comment