Msanii muziki katika game ya Bongo aliyekuja kwa kasi kubwa na kupotea, Harmorapa maarufu kwa jina la mzee wa kutafuta Kiki amedai hajaishiwa kiki kama wengi wanavyosema.
Harmorapa ameeleza kuwa ukimya wake unasababishwa na biashara anazofanya nje ya muziki pamoja na show zake za mikoani ambazo amekuwa akifanya mara nyingi.
''Nipo bize sana na mishe nyingine nje ya muziki, namaanisha mimi ni mfanyabiashara, so huwa mara nyingi nasafiri, mara nyingi huwa napiga tour zangu mikoani na project zangu za muziki zipo kama kawaida'' amesemaHarmorapa .
Amefunguka pia kutokana na hilo ni vigumu sana kumkuta Dar es Salaam kwani anakuwa bize sana.
Harmorapa Ft Cpwaa & Ronei - Nundu {Official Video}
No comments:
Post a Comment