Mwanamuziki Baraka The Prince Afungukia Issue Ya Kumuomba Msamaha Alikiba - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, 26 October 2017

Mwanamuziki Baraka The Prince Afungukia Issue Ya Kumuomba Msamaha Alikiba


Msanii wa muziki Bongo Flava, Barakah The Prince amefunguka ishu ya kumuomba msamaha Mkongwe kwenye game ya Bongo Flava Alikiba.


Barakah The Prince ambaye aliondoka katika label ya RockStar4000 baada ya Alikiba kuwa miongoni mwa mabosi wa label hiyo ameiambia Planet Bongo ya EA Radio kuwa wao hawajawahi kugombana hivyo suala la kuomba msamaha halipo.
''Mimi na Alikiba hatuna tatizo, tuna muda tu hatujawasiliana lakini sijawahi kuwa na tatizo naye isipokuwa watu wanaforce mimi kuwa na matatizo naye, inaweza kuwa ni mashabiki, pia watu wake wa karibu'' alifunguka hivyo Barakah The Prince.
Ameongezea kuwa tangu aondoke RockStar4000  hawajawasiliana Yeye na Alikiba na hawana tatizo ila ni kwamba mara nyingi akimpigia simu Alikiba huwa hapokei.

Barakah Da Prince Ft Alikiba - Nisamehe {Official Video}

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here