Rapper Bill Nass azidi kuitamani Kolabo na Alikiba - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, 24 October 2017

Rapper Bill Nass azidi kuitamani Kolabo na Alikiba


Rapper Bill Nass {Nenga a.k.a Mzungu Mzee} amefunguka kuwa bado nia yake ya kufanya kolabo na msanii Alikiba ipo pale pale.

Bill Nass {Nenga} ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ''Sina Jambo'' ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa uwezo wa Alikiba kubadilika kwenye kila kolabo ndio unamshawishi kufanya hivyo.

''Ikiwezekana kwa sababu ni mmoja kati ya watu ambao nawaona, kolabo ambazo amewahi kufanya mapokezi yake ni Makubwa, yuko flexible kwenye collaboration anafaa'' amesema Bill Nass.

''Alikiba ni moja kati ya wasanii ambao wamenishawishi kufanya nae kazi kwa sababu ana muda mrefu kwenye game nimekuwa nikimsikia nikiwa bado hata sijafikiria kufanya muziki lakini bado anafanya vizuri, ngoma kama Seduce Me nimeiona mbali sana nimependa production yake'' ameongeza.

Mwana FA, Godzilla na Mr. Blue ni miongoni mwa wasanii wanaofanya muziki wa rap ambao waliweza kumshirikisha Alikiba katika ngoma zao na aliweza kuzitendea haki chorus za ngoma hizo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here