Rosa Ree Amefunguka Kitu Ambacho Awezi kuacha Kwenye Muziki wake - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, 26 October 2017

Rosa Ree Amefunguka Kitu Ambacho Awezi kuacha Kwenye Muziki wake


Msanii anaefanya vizuri kwenye game ya Hip hop Bongo Rose Ree amefunguka ni vigumu kuacha kutumia lugha ya kingereza katika ngoma zake kwani muziki ni vile ambavyo mtu anataka kujielezea na si vinginevyo.

Rapper huyu ameendelea kwa kusema si kwake tu bali hata kwa wasanii wengine wanaweza kutumia lugha yoyote Lengo ni kufikisha kwa jamii kile ambacho wanakitaka kwa wakati huo.
''Huwezi kum-limit mtu kutumia lugha fulani katika muziki, kwani ni chombo cha kujielezea unavyohisi na kuelezea hisia zako kwa wakati ule, kwa hiyo kama wewe unahisi hisia zako zinakuambia imba kilugha fanya hivyo, kwa hiyo mimi hisia zangu ndio zinajielezea katika lugha ambazo natumia'' Rosa Ree amefunguka ivyo.
''Ndio maana hata kwenye Up In The Air nilisema, watu walikuwa wanasema huyu demu anarap sana kingereza sana hajui Kiswahili nikawaambia siwezi Kiswahili nitakupa na kichaga kwa sababu kipaji cha Rosa Ree kinavuka mipaka is not about language'' Rosa Ree ameongeza.
Kwa sasa Rosa Ree anafanya vizuri na ngoma yake mpya Dow baada ya kufunika vilivyo na ngoma Up In The Air.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here