Rapper Kutoka Crew ya Muziki wa Hip Hop SSK, {Sisi Sio Kundi} ZaiiD amefunguka kuwa si kweli kwamba style ya G-Nako ya kuimba na kurap katika game ilimshawishi kufanya ngoma yake ya ''Umeme Umerudi''.
Rapper ZaiiD amefunguka kuwa chimbuko la ngoma hiyo ni kutokana na yeye kusikiliza aina nyingi za miziki tofauti lakini anaheshimu anachofanya G-Nako katika game ya Bongo Flava.
''Hapana, mimi pia ni shabiki wa aina nyingi za rap, sijui kwa sababu G-Nako naye amefanya, Marehemu Arbert Mangwea alikuwa anaimba na kuchana, Chidi Benz Pia Hivyo hivyo, Mimi nilikuwa nikisikiza miziki mingi sana'' ZaiiD amefunguka ivyo
''Namuheshimu G-Nako kwa anachofaya kwenye game ila hakuni-inspire kufanya Umeme Umerudi, niliamua kwa sababu nilihisi ni muda halisi wa kuongea vitu ambavyo vitasika mwanzo hadi mwisho kwa ukaribu na urahisi'' ameongeza.
ZaiiD kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ''Wowowo'' pamoja na ile ya kundi {SSK - Slow Down}.
No comments:
Post a Comment