Kala Jeremiah Amefunguka kuhusu Wasanii wa Hip Hop ambao mashairi yao hayazingatii rika. - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, 28 July 2016

Kala Jeremiah Amefunguka kuhusu Wasanii wa Hip Hop ambao mashairi yao hayazingatii rika.

                        
Msanii wa miondoko ya Hip Hop nchini, Kala Jeremiah anaetamba na ngoma yake ya ''Wanandoto''
amefunguka kuwa wasanii wengi wengi wa Hip Hop nchini wanashindwa kueleweka kwa mashabiki
wa muziki wa rika zote kutokana na namna wanavyopangilia mashairi bila kujali rika la wanaosikiliza muziki huo.

Kupitia kipindi cha Plannet Bongo, Kala amefunguka kuwa akiandika mashairi, jambo la kwanza kujiuliza kama Babu au Bibi anaweza kuelewa ujumbe aliouweka ndani ya wimbo huo, Pia amezungumzia Nyimbo yake mpya ya ''Wanandoto''  kuwa ni wimbo ambo ameuimba kuhamasisha jamii kuwa watoto wanapaswa kuthaminiwa ili waweze kutimiza ndoto zao.

''Nyimbo zangu kila ninapoenda hadi wazee wanaziimba ni kutokana na mpangilio wa mashairi na ujumbe unaoihusu jamii ambayo unakuta nimeielezea vizuri'' Amesema Kala Jeremiah.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here