Mambo 4 anayotakiwa kufanya Nay wa Mitego ili aruhusiwe tena kufanya sanaa. - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, 27 July 2016

Mambo 4 anayotakiwa kufanya Nay wa Mitego ili aruhusiwe tena kufanya sanaa.

               


Leo Jumatano ya July 27 Balaza la Sanaa Tanzania limetangaza rasmi kumfungia msanii Nay wa Mitego kujihusisha na sanaa kwa muda usiojulikana.Hiyo inatokana na msanii uyo kuachia
zisizokua na maadili ya kitanzania ikiwa sio mara ya kwanza kuonywa na balaza hilo ila
msanii uyo ameonekana kutofata sheria na taratibu alizopewa na balaza hilo.

Wiki tatu zilizopita msanii nay wa Mitego aliachia nyimbo yake inayoitwa ''Pale kati Patamu''
nyimbo ambayo ilizua gumzo mtaani kutokana na maneno yaliotumika katika nyimbo hiyo
hayakua ya kimaadili kwa namna moja ama nyingine na hivyo kuchukua muda mchache na kisha
kufungiwa na BASATA.

Amlifaya ya Clouds FM imepiga story na Godfrey Mungereza kutoka BASATA na ameweka wazi
kuhusu taarifa hiyo ya kufungiwa kwa Nay wa Mitego na akayataja masharti ambayo wamempa
msanii huyo endapo akiyatekeleza wanaweza kumuachia akaendelea kufanya kazi zake za sanaa.

Mambo hayo ambayo anatakiwa kuyatekeleza Nay wa Mitego ni

1. Kulipa faini ya Tsh Milioni 1

2. Kufanya marekebisho ya mashairi katika wimbo wake wa ''Pale kati Patamu''

3. Aombe radhi katika jamii

4. Ajisajiri rasmi kama msanii alie chini ya baraza hilo.

Hayo ndio mambo ambayo anayotakiwa kuyatekeleza Nay wa Mitego, huenda tukamsikia tena
hewani wowote kama atatekeleza mambo hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here