Mkali wa Music wa RnB Steve RnB atoa dongo hili kwa wasanii wenzake Nuruelly na Rama Dee - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday, 5 November 2016

Mkali wa Music wa RnB Steve RnB atoa dongo hili kwa wasanii wenzake Nuruelly na Rama Dee

Image result for Steve RnB 2016
Msanii Mkali katika muziki wa RnB nchini Steve RnB amesema hawezi kufanya muziki wa kisingeli na siku akifanya atachekesha hata Nuruelly na Rama Dee wamekosa washauri sahihi mpaka kuamua kufanya aina hiyo ya muziki.

Akipiga story ndani ya eNewz, amesema hadhani kama ni kitu sahihi kutoka katika muziki wa RnB na kuimba Singeli labda kama waliofanya hivyo walifanya kwa kutafuta mashabiki pamoja na kufanya mashabiki kumsikiliza kwa karibu kwa kuwa walikaa kimya kwa muda mrefu.

Hata hivyo alimsihi Nuruelly kutafuta washauri wazuri ili kuweza kufanya muziki mzuri kwa kuwa yeye anaamini kuwa Nuruelly anaweza akafanya muziki mzuri na ana sauti nzuri pia ni mtunzi mzuri sana wa nyimbo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here