Alichokisema Madee juu ya shutma za kuvaa nguo yenye mfano wa SANDA Kwenye Fiesta Mwanza! - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday, 24 August 2016

Alichokisema Madee juu ya shutma za kuvaa nguo yenye mfano wa SANDA Kwenye Fiesta Mwanza!

 
Kama ulifanikiwa kuitupia jicho show aliyoifanya Madee katika jukwaa la Fiesta mkoani Mwanza pande za CCM Kirumba utakuwa alijiuliza mara mbilli kutokana na muonekano wa kimavazi wa msanii huyo wakati akiingia jukwaani.

Ni kitu ambacho kiliwashangaza wengi kutokana na msanii huyo kuvaa vazi ambalo lina muonekano kama Sanda. Lakini kwa upande wake lilikuwa na maana vazi hilo.

Baada ya 255 kumsaka Madee na kupiga nae story haya ndio yalikuwa majibu yake baada ya comments za mashabiki kuwa nyingi.

''Mimi ndio nilipeleka idea ya kutengenezewa nguo yenye muonekano kama ule, na lengo langu lilikuwa ni kufikisha maana fulani katika jamii. Wakati naingia pale stejini ilikuwa ni giza, na nilivaa nguo nyeupe nkiwa nina maana ya kwamba hata mtu angekuwa kwenye giza kiasi gani basi ataweza kuona pale kuna kitu cheupe kina ng’aa. Nikiwa namaanisha kwamba mimi nipo kwenye giza na kuna baadhi ya watu hawaoni umuhimu wangu, hawaoni nini nafanya lakini mimi ni mweupe hata niwe kwenye giza kiasi gani lazima nitaonekana.''

cloudsfmtz-20160824-0002

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here