Ben Pol kutupa karata kwenye muziki wakurap kwa style hii. - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday 9 August 2016

Ben Pol kutupa karata kwenye muziki wakurap kwa style hii.

 Ben Pol
Msanii wa muziki wa R&B Bernard Paul aka Ben Pol amesema ukifika wakati aachia wimbo mmoja wakurap ili kuonyesha uwezo wake.

Muimbaji huyo ambaye ameachia wimbo ‘Shilingi’ akiwa na Stereo, ameiambia Bongo5 kuwa kama akiamua kutoa wimbo wa kuchana, atachana mistari minne tu katika wimbo mzima.

''Mimi naweza kuchana, alisema Ben Pol ''Kwa hiyo kama ngoma yakuchana ukifika wakati nitafanya lakini sio wimbo mzima, labda mistari mine tu alafu sehemu nyingine nitaimba kama kawaida,''

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake ''Moyo Mashine'' ambao umeshika nafasi ya kwanza katika vituo mbalimbali vya radio na runinga.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here