Msanii Darasa ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake ya 'Too much' amefunguka na kumuelezea Roma Mkatoliki kuwa ni mtu ambaye yupo naye karibu na anamchukulia kama braza wake kwani hata familia zao zinawatambua kuwa ni watu wa karibu ambao wamekuwa wakisaidiana na kushauriana.
Darasa anasema anaona ni heshima yeye kuwa katika collabo ya Roma Mkatoliki katika wimbo wake wa
'Kaa Tayari' ambao pia ameshiriki Jose Mtambo, Darasa anasema anashukuru namna mashabiki wameweza kuwapokea.
''Kwanza kabisa mimi na Roma ni kama mabraza ambao tunashauriana mengi, mimi nimeanza kufanya vizuri namkuta Roma kwenye game anafanya vyema, lakini mpaka sasa Mama Roma na familia ya Roma inamjua vyema Darasa sababu sisi ni washikaji wa karibu, lakini kingine mimi kuwepo kwenye kazi moja na Roma Mkatoliki nachukulia kama heshima kwangu na tunashukuru kwa mashabiki zetu ambao wameweza kutupokea vyema'' alisema Darassa.
No comments:
Post a Comment