DULLY SYKES: Mimi nina sikio la muziki, HARMONIZE yuko tofauti, kwanza hajazaliwa na koo la DIAMOND. - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Saturday 13 August 2016

DULLY SYKES: Mimi nina sikio la muziki, HARMONIZE yuko tofauti, kwanza hajazaliwa na koo la DIAMOND.

 
Msanii mkongwe wa Bongo fleva Tanzania,Dully Sykes amesema haoni kama Harmonize anafanana na Diamond kwenye kuimba kama watu wengi wanavyosema.

Akihojiwa kwenye kipindi cha Friday night live cha East Africa Television,Dully pia amedai kuwa sio vibaya kama Harmonize anafanana na Diamond kwa sababu ndiye aliyemkuza kimuziki kwani watu wakikaa pamoja kwa muda mrefu hufanana.

''Mimi nina sikio la muziki,Harmonize yuko tofauti,kwanza hajazaliwa na koo la Diamond.Lakini wanamfananisha Harmonize kwa sababu ameishi sana pamoja na naye,lazima mtafanana, Hata mimi kuna wasanii nimeishi nao wana pozi kama mimi,pia Harmonize amefikishwa mbali na Diamond kama ataamua kumfuata anavyofanya sio mbaya.Wakati mwingine kuna ukweli kuwa anafanana na Diamond kwa sababu amekua kwa Diamond,sasa mnataka afanane na nameless au?

Alihoji Dully Sykes wakati akitambulisha video yake mpya alivyofanya na Harmomize kwenye kipindi hicho cha Friday Night kinachoruka kila ijumaa kuanzia saa tatu usiku.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here