Fahamu zaidi kuhusu ''SISI'' kundi jipya la muziki linalo undwa na Nikki Mbishi, Stereo na One the Incredible.. - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Sunday 7 August 2016

Fahamu zaidi kuhusu ''SISI'' kundi jipya la muziki linalo undwa na Nikki Mbishi, Stereo na One the Incredible..

 Wiki iliyopita wakali Nikki Mbishi, Stereo na One the Incredible waliachia ngoma yao ya pamoja inayoitwa “SISI” nyimbo ambayo walimshirikisha Godzilla.

Masaa machache baadae waka bonga na 255 ya Clouds Fm kuwa wamefikia maamuzi ya kuliunda kundi ambalo wamelipa jina la SISI, kundi ambalo linaundwa na wasanii ambao walitoka chini ya Record label ya M-Lab kwa Producer Duke.

Baada ya miaka zaidi ya 4 kupita ambapo kila mmoja alisimama kama solo artist baada ya kutoka katika mikono ya Duke wakali hao wameona haita kuwa vibaya wakiunganisha nguvu na kufanya kitu kimoja ambacho ni Fantastic.

255 ikaona imkamate  Nikki Mbishi atusanue kuhusiana nahili.

''SISI imekuja kipindi ambacho ule usemi wa umoja ni nguvu utengano ni udhaifu umeanza kudhihirika, kwasababu watu wengi waliokuwa na nguvu katika makundi leo hii nguvu zao zimepungua, nakutolea mfano hai kundi kama East Coast lilikuwa lina wasanii wengi ambao wanafanya vizuri, lakini waliobakia wanafanya vizuri  mpaka sasa ni wachache. Sisi pia tulisha wahi kufanya vizuri, Mimi nina brand yangu, Incredible ana brand yake na Stereo pia ana brand yake! Kwanini tusiunganishe nguvu na tukafanya kitu kikubwa!? Kwahiyo tumeamua kuunda joint ambayo itafanya twende mbele zaidi.'' Ni baadhi ya majibu ya Nikki Mbishi.

Unaweza kuisikiliza Nikki Mbishi kwenye Interview hapa chini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here