Baada ya kuachia ngoma ya ''Kazi Kazi'' aliyoshirikiana na Sholo Mwamba, Profesa Jay ameamua kufunguka juu ya mashabiki wa singeli pamoja na wasanii wake wanaoimba muziki huo.
Jumaa Lunduno amekosegezea moja ya maongezi ya Profesa Jay ambayo ameamua kufunguka juu ya muziki wa Singeli baada ya kufanya kazi na mmoja ya wasanii wa muziki huo.
Profesa Jay alisema kwamba aliimba ngoma ya ''Kazi Kazi'' kwa ajili ya kufikisha ujumbe katika jamii vilevile na kuamua kuchukua fursa katika muziki wa singeli ili kuwatoa watu hofu kuwa muziki wa singeli sio wakihuni.
''Lakini pia kuleta mapinduzi naona pia kuna fursa katika muziki wa Singeli, kwahiyo namimi nikishiriki naona labda watu wataelewa huu mziki sio wa kiuni, japokuwa kunawahuni ambaopia wanafanya muziki huo, kwahiyo nikawa nawaambia mashabiki wa singeli watu wanashindwa kuwekeza kwasababu mnabeba mapanga na bisibisi, inabidi watumie lugha ambazo ni nzuri, watu show zao wauzurie na hata watu wenye heshima pia waweze kuhudhuria, Maana wakina Sholo Mwamba, Manfongo wakipata Fursa wanaweza kuajiri watu wengine kama walivyo wakina Diamond na Alikiba.'' Alisema Profesa Jay.
No comments:
Post a Comment