Stamina: Ujumbe kwa Artist Wenzangu.. - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Wednesday 3 August 2016

Stamina: Ujumbe kwa Artist Wenzangu..

 
Baada ya kuachia ngoma yake jana ya “Mmeniroga remix” aliyofanya na Jay Mo na Roma, Stamina ameandika ujumbe kwa ma Artist wenzake.

 Kupitia kurasa ya Instagram ya Stamina amefunguka kuwa chanzo cha matabaka kwa wasanii ni kutokupeana tafu wenyewe kwa wenyewe katika muziki, ambo amesema unakuta msanii anamwomba msanii mwenzie ampostie cover ya nyimbo au show unakuta huyo msanii anakausha.

 “Tabia ya kutopeana tafu wenyewe kwa wenyewe ndio inaleta matabaka kwenye mziki, Mwenzako anashow sehemu au ana nyimbo yake mpya anakutumia Cover ya wimbo au show yake unaipata kabisa ila hutaki kuiposti tu. Cha ajabu za wengine ambao ndio unawaamini washkaji zako unaziposti fresh tu kwa mbwe mbwe zote. Mtu mpaka ana namba yako maana yake tayari mnajuana na mna ukaribu pia, hata kama hamna ukaribu ila ni sababu msanii mwenzie we mpe supprt tu” Aliandika Stamina.
 Stamina aliongeza pia kuwa kuna baadhi ya wasanii wao wenyewe wanasubilia mpaka msanii mwenzake apigike kimaisha, afe au anatumiwa dawa ndio aanze kumposti.

 “Mnasubiri mpaka mtu afariki/afe ndo mnajifanya kuposti R.I.P wakati hawezi hata kuiona hiyo post yako, Mnsasubiri mpaka mtu awe ameathirika na madawa, au kapigika kimaisha ndo mnajifanya kupost picha au clip vya video na kujifanya mnahuzunika. Me nikifa kausha tu usiposti maana sitaona wala haitosaidia kama kipindi niko hai” Stamina.

 Unalizungumziaje ishu hii ya stamina

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here