Dogo Janja ajing’ata ng’ata kuhusu Siwema wa Nay wa Mitego - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Monday, 12 September 2016

Dogo Janja ajing’ata ng’ata kuhusu Siwema wa Nay wa Mitego


Wimbo wa My Life kutoka kwa Dogo Janja ni miongoni mwa ngoma ambayo mashabiki wengi
walidhani hata weza kufanya wimbo mwingine ukaushinda huo, Lakini msanii huyu ameachilia ngoma mpya ya Kidebe na kuwa gumzo mtaani kutokana na kuwasifia maadhi ya wasanii huku akiwaponda wengine.

eNEWZ ilitaka kufahamu kuhusiana na chanzo cha Dogo janja kumsema Siwema ambaye anajulikana alikuwa ni mpenzi wa rapa Nay Wa Mitego na kubahatika kuzaa naye mototo mmoja ambapo alisema ''Sio kiburi sio mchafu kama Siwema''.

Dogo Janja aliamua kujitetea kuwa sio Siwema wa Nay wa Mitego bali ni msichana mwingine kutoka Arusha mtaa wa Ngarenaro, Pia alifafanua zaidi hata wapo wengi wanao itwa Dogo Janja lakini sio Dogo janja yeye.

''Mimi sijamzungumzia Siwema wa Nay wa Mitego, Siwema pale mtaani kwetu Ngarenaro kuna mwanamke anaitwa Siwema. Anatabia za kimiyeyusha yani sio mchoyo watu wengi wanapaa sana'' Alisema Dogo Janja kufafanua mstari wake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here