Dogo Janja -: Sijamuimba Siwema wa Nay wa Mitego! - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Thursday, 8 September 2016

Dogo Janja -: Sijamuimba Siwema wa Nay wa Mitego!


''We mzuri we mkali kama Wema, sio kuburi sio mchafu kama Siwema” ni mistari ya Dogo Janja ambayo inapatikana kwenye ngoma yake mpya inayofahamika kama ''Kidebe''.

Mistari hiyo imezua gumzo kubwa sana mtaani na wengi kufikiria kwamba Dogo Janja amemuimba aliyekuwa mpenzi wa msanii Nay wa Mitego ambaye anaitwa Siwema.

Dogo Janja amekanusha maneno hayo na kidai kwamba Siwema aliyomzungumzia yeye ni Siwema wa mtaani kwao Ngarenaro, sababu ni demu flani hivi mwenye sifa kama zilizo zungumzwa na Jux pamoja na  Yong Dee kwenye ngoma ya ''Sio Mchoyo''. Yani vijana wengi wa mtaani kwao wamesha mkwaa dem huyo.

 Dogo Janja alitoa mfano hai kwa kusema kwamba ''Leo hii ukisema Boya kama Dogo Janja, kuna kina Dogo janja wengi sana mtaani ila mwisho wasiku aliyesimama imara na jina hilo ni mimi na watu wengi wanaweza kuchukulia hilo kama umeni-diss mimi”.

Itazame hapa video ya ''Kidebe'' ya Dogo Janja


http://www.srv33.youtubeinmp4.com/download.php?r=GJFPbIfUbJUhPCOBxQ%2BtWI%2B2gbj0WTOYFXyUPh%2BF%2F0LZI2Q04Byi3gYNVfv%2Bc7Xw42EmZBZK8uFMUGm6eZvvnOglpivZN8c5JZkZxdoSMzUD89%2BocDV6M%2B4mGdIjHw9P061IJoz1lJE9R0Km0n9E5s%2FU2FUBT91YPEOb67u%2BBtU%3D

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here