Ommy Dimpoz:- Wasanii wa sasa tunaendeshwa na presha za mashabiki - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, 15 November 2016

Ommy Dimpoz:- Wasanii wa sasa tunaendeshwa na presha za mashabiki

 Image result for Ommy Dimpoz
 Ommy Dimpoz Ameamua kuvunja ukimya na kufunguka kuzungumzia ushindani uliopo kwenye muziki wa sasa na kipindi ameingia kwenye tasnia hiyo.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo wa 'Kajiandae' akiwa na Alikiba amesema kuwa presha za mashabiki ndio zinasababisha nyimbo za wasanii kupotea mapema na kuwafanya waachie nyimbo nyingi kwa muda mfupi tofauti na zamani ilivyokuwa.

''Unajua ushindani wa sasa hivi na wazamani umebadilika. Zamani ulikuwa unaweza kutoa wimbo kwa muda mrefu ukakaa lakini sasa hivi imekuwa watu wiki nyimbo, wiki nyimbo japo mimi siupendi sana huo utaratibu kiukweli,'' Ommy Dimpoz amezungumza na  kipindi cha The Playlist cha Tmies FM na kuzungumza maneno hayo.

''Naona si utaratibu mzuri kwa sababu hauzipi nyimbo zako nafasi, unainvest matokeo yake nyimbo zinakufa mapema. Tusifanye nyimbo kwa presha yaani sometimes mashabiki pia wanatupa presha sana, inabidi waelewe kwamba kuna kuinvest hela nyingi, shabiki anachotaka yeye raha umridhishe lakini pia shabiki anatakiwa aelewe video zinacost hela nyingi,'' Aliongezea kwa kusema ivyo.

Ommy Dimpoz ameongeza kuwa walau msanii kuwa wanatakiwa atoe nyimbo kila baada ya miezi mitatu ili kuzipa nafasi nyimbo zake nyingine zilizopita.
 Image result for Ommy Dimpoz kajiandae
Ommy Dimpoz

Download hapa | New Music Audio & Video | Ommy Dimpoz - Kajiandae

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here