Darassa CMG aweka wazi lengo lake kubwa kwenye muziki wake - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday 6 December 2016

Darassa CMG aweka wazi lengo lake kubwa kwenye muziki wake

Related image 
''Maisha na Muziki'' ni ngoma ambayo imetoka kwa kipindi kifupi na kuweza kuteka hisia za kila mtu yaani Muziki imekuwa ni ngoma flani ambayo sasa hivi kila ukipita sehemu kila mtu utasikia maisha na Muziki.

Rapper anayefanya vizuri kwa sasa kwenye muziki wa Hip Hop, Darassa amefunguka juu ya malengo aliyonayo kwenye ramani ya muziki wake hapa nchini.

Darassa amekiambia kipindi cha Dj Show cha Radio One,  
''Lengo langu si kuamka asubuhi watu wakasema mimi ndio best rapper au mimi ninaweza kuwa mkali kwenye hiki kipindi, lengo langu ni kuweka historia kwenye muziki wangu hata kama nisipotoa wimbo historia yangu ibaki inafanya kazi. Naomba Mungu anisaidie sana kwa hili.''

''Nafikiri Too Much inahitaji wimbo mwingine kwa sababu toka nimeutoa hakuna wimbo mwingine unaweza kukaa juu ya wimbo huo. So hakuna sababu ya sisi kuendelea kusubiri mashabiki wetu wanahitaji burudani, ndio sababu kubwa imepelekea kuleta project hii mpya.''

Rapper huyo ameongeza kuwa wimbo wake mpya wa Muziki ambao mpaka sasa umetazamwa zaidi ya mara 801k kwenye mtandao wa Youtube umetayarishwa na maproducer watatu akiwemo Mr VS, Mr T-Touch na Abbah wa Abbah Process.

Downloada New Music Audio & Video Dara Feat Ben Pol - MUZIKI



No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here