Nay wa Mitego: Sioni msanii wa kumfananisha na Alikiba kwenye kuimba - Jumaa Lunduno

Post Top Ad

Responsive Ads Here

Tuesday, 24 January 2017

Nay wa Mitego: Sioni msanii wa kumfananisha na Alikiba kwenye kuimba

Inafahamika fika kuwa Nay wa Mitego ni mmoja kati ya wasanii ambao ni marafiki wa karibu sana wa msanii Diamond Platnumz.

Hivi kuna ambaye hafahamu kama Diamond Platnumz na Alikiba hawana maelewano mazuri? Sasa chukua hii exclusive kutoka kwa Nay wa Mitego.

Nay wa Mitego amepaza sauti kupitia kipaza cha 255 na kudai kuwa haoni msanii wa kumfananisha na Alikiba katika suala zima la kuimba.

''Wasanii ni wengi, me mmoja kati ya wasanii ambao nawaelewa sana kwenye suala la uimbaji ni pamoja na Alikiba, Alikiba ni muimbaji mzuri sana, nafikiriaga mtu wa kumuweka karibu nae simpatagi.'' Alisema Nay wa Mitego.

Kuirefu zaidi play hii video hapa chini kumsikiliza Nay wa Mitego akimwaga sifa hizo kwa mkali King Kiba.

WATCH VIDEO

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Responsive Ads Here