Umeshawahi kufikiria kuhusu Dogo Janja kuwa na lebo yake mwenyewe kisha msanii wa kwanza kumsainisha akawa ni ya Young Killer? Sasa fikiria itakuwaje endapo ikitokea.
Msanii Dogo Janja a.k.a Janjaro kutoka kundi la Tip Top Connection amekuwa na Ndoto siku moja ya kuja kumiliki Lebo yake ya Muziki kama Wasanii wengine wakubwa wanavyofanya.
Kupitia kipindi cha Friday Night Live (FNL), Dogo Janja adai endapo angekuwa tayari anamiliki lebo yake na msanii wa Kwanza aliyemtaja kumsaini kwenye Lebo hiyo angekuwa ni Young Killer.
Dogo Janja anaewafurahisha mashabikli wake na wimbo wake wa ''Kidebe''
Alisema ''Young Killer ni msanii mkali lakini anahangaika sana kutoboa hivyo angemsaini ili kufikia malengo yake''.
No comments:
Post a Comment